# Sentensi unganishi Yesu anaendelea kufundisha jinsi alivyokuja kutimiliza sheria za agano la kale. Hapa anaanza kufundisha juu ya kuua na hasira # Maelezo kwa ujumla Yesu anawaambia kikundi cha watu juu ya kile ambacho kinaweza kutokea kwao kama watu binafsi. Neno "mme" katika sentensi "mmesikia" na "nawaambia" ni maneno ya wingi. Ile amri ya "usiue"ni ya umoja, lakini unahitaji kuitafsiri katika wingi. # ilinenwa zamani Hii inaweza kuelezeka kwa mfumo tendaji. "Mungu alisema na mababu zetu zamani za kale". # auaye yuko katika hatari ya hukumu Hapa "hukumu" inamaanisha kuwa hakimu ndiye atakayemhukumu mtu kufa. "Hakimu atamhukumu yeyote amuuaye mtu mwingine" # kuua ... auaye Neno hili linamaanisha kitendo cha mauji ya kudhamiria, na wala siyo kila aina ya mauji # Lakini nawambia Kiwakilishi "na" kinatia msisitizo. Hii inamaanisha kuwa kile anachosema Yesu kina umuhimu sawa na amri itokayo kwa Mungu. Jaribu kutafsiri hili kataka mazingira yanayonesha msisitizo. # ndugu Neno hili linamaanisha muumini mwenzetu # atakuwa katika hatari ya hukumu Inaovyoonekana hapa Yesu hamaanishi hakimu wa kibinadamu bali Mungu anamhukumu mtu mwenye hasira kwa ndugu yake. # mtu usiyefaa ... mjinga Hii ni mizaha kwa watu wasioweza kufifkiri kwa usahihi. "Mtu asiyefaa" ni sawa na "mtu asiye na akili," ambapo "mjinga" inaongezea wazo la kutokuwa mwaminifu kwa Mungu. # baraza Yawezekana hili ni baraza dogo, siyo lile kuu.