# Sentensi unganishi Yesu anamaliza kueleza tabia za watu ambao wamebarikiwa. # Mliobarikiwa Neno "ninyi" ni wingi. # kusema kila aina ya mambo maovu dhidi yenu kwa uongo. "watasema kila aina ubaya dhidi yenu" au "watasema mambo mabaya juu yenu ambayo si ya kweli" # kwa ajili yangu "kwa sababu mwanifuata mimi" au "kwa sababu mwaniamini" # Furahini na kushangilia "Furahini" na "kushangilia" humaanisha karibu kitu kile kile. Yesu alitaka wasikilizaji wake sio tu kufurahi bali hata kufanya zaidi kuliko kufurahi kama inawezekana.