# Taarifa kwa ujumla: Huu ni mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi ambayo katika hiyo mwandishi anaeleza mwanzo wa huduma ya Yesu Galilya. Mistari hii inaeleza jinsi Yesu alivyokuja Galilaya # Sasa Neno hili lintumika hapa kuweka alama ya kuanzisha mtiririko wa habari kuu wa simulizi. Hapa Mathayo anaanza kutuambia sehemu mpya ya simulizi. # Yohana alikuwa amekamatwa Hii inaweza kuelezwa katika namna ya muundo tendaji. "mfalme alikuwa amemkamata Yohana." # Katika majimbo ya Zabuloni na Naftali Haya ni majina ya makabila ambayo yaliishi katika maeneo haya kabla ya wageni kudhibiti nchi ya Israeli miaka mingi kabla.