# Maelezo yanayounganisha Huu ni mwisho wa sehemu ya simulizi kuhusu Yohana Mbatizaji na hueleza kilichotokea baada ya kumbatiza Yesu. # Baada ya kubatizwa Hii inaweza kueleza katika namna iliyo tendaji. "Baadaya Yohana kumbatiza Yesu" # tazama Neneo "tazama" hapa hututahadharisha sisi kuwa makini kwa habari ya kushtukiza ambayo inafuata. # mbingu zilifunguka kwake Hii inaweza kuelezwa katika namna iliyo tendaji. "Yesu aliona mbingu zimefunguka" au "Mungu alizifungua mbingu kwa Yesu." # kushuka chini kama njiwa Maana zinaweza kuwa 1) haya ni maelezo dhahiri kwamba Roho alikuwa katika umbo la njiwa au 2) huu ni mfanano ambao hulinganisha Roho kushuka chini kuja juu ya Yesu kwa upole, ndivyo njiwa angefanya. # sauti toka ilitoka mbinguni ikisema "Yesu alisikia sauti kutoka mbinguni." Hapa "sauti" humaanisha Mungu anazungumza. "Mungu alizungumza kutoka mbinguni." # Mwana Hiki ni cheo cha maana cha Yesu, Mwana wa Mungu