# Maelezo yanayounganisha Hapa mandhari yahamia kwenda wakati wa baadaye wakati Yohana Mbatizaji ambatiza Yesu. # kubatizwa na Yohana Hii inaweza kueleza katika namna iliyo tendaji. "hivyo Yohana aliweza kumbatiza." # Nina hitaji kubatizwa wewe, nawe waja kwangu? Yohana anatumia swali kuonesha kushangazwa kwake na ombi la Yesu. "Wewe ni wa maana zaidi kuliko mimi. Sipaswi kukubatiza wewe. Wewe unapaswa kunibatiza mimi." # kwa ajili yetu Hapa "sisi" humaanisha Yesu na Yohana.