# Sasa...asali ya nyikani Neno "sasa" limetumika hapa kuweka alama kutenganisha mtiririko mkuu wa simulizi. Hapa Mathayo ana simulia habari za historia ya nyuma kuhusu Yohana Mbatizaji. # alivaa nguoa za manyoa ya ngamia na mkanda wa ngozi katika kiuno chake. Vazi hili huashiria kwamba Yohana ni nabii kama manabii wa tangu zamani, hususan nabii Eliya. # Kisha Yerusalemu, Uyahudi yote, na mkoa wote Hii humaanisha watu kutoka maeneo yale. "Hapa neno "yote" humaanisha "wengi." Mathayo anasisitiza jinsi watu wengi walivyoenda kwa Yohana Mbatizaji. # Walibatizwa naye Hii inaweza kuelezwa katika namna iliyo tendaji. "Yohana aliwabatiza." # Wao Hii inamaanisha watu waliokuja kutoka Yerusalemu, Uyahudi, na mkoa kuzunguka Mto Yordani.