# Amoni Wakati mwingine jina hili limetafsiriwa "Amosi" # Yosia alikuwa baba wa Yekonia Yosia alikuwa kwa kweli babu yake na Yekonia. # wakati wa kuchukuliwa kwenda Babeli "wakati walipoamriwa kwa nguvu kuondoka kwenda Babeli" au "wakati Wababeli walipo washinda na kuwahamisha kwenda kuishi Babeli." Kama lugha yako inahitaji kuwataja wazi ambao walienda Babeli, unaweza kusema "Waisraeli" au Waisraeli ambao waliishi Yuda. # Babeli Hapa humaanisha nchi ya Babeli, sio tu mji wa Babeli.