# Wakanyanyuka Inahusiana na wale watu wawili # nyanyuka "kuamka" au "kusimama" # wale kumi na moja Hii inaongelea wale mitume wa Yesu. Yuda hakuwa pamoja nao. # wakisema, "Bwana amefufuka kwelikweli Wale mitume kumi na moja na wale waliokuwa pamoja nao walisema hivyo. # Hivyo wakawaambia "Hivyo wale watu wawili wakawaambia" # mambo yaliyotokea njiani Hii inamaanisha Yesu alivyowatokea wakiwa njiani kuelekea kijiji cha Emmau. # namna Yesu alivyodhihirishwa kwao Tafsiri mbadala: "namna walivyomtambua Yesu" # katika kuumega mkate "wakati Yesu alipouvunja mkate" au "wakati Yesu alipouchana mkate"