# Ilitokea Hii sentensi ilitumika hapa kuweka alama ya tukio muhimu katika simulizi. # mavazi ya kung'aa "wamevaa angavu, mavazi yanayong'aa" # wamejaa hofu "wakaogopa" # Kwanini mnamtafuta aliye hai miongoni mwa wafu? Wale wanaume wanatumia swali kuwapinga wale wanawake kumtafuta kwenye kaburi mtu aliyehai. Tafsiri mbadala: " Mnamtafuta mtu aliye hai kati ya au miongoni mwao wafu" au "Hamtakiwi kumtafuta mtu ambaye yu hai katika sehemu wanapozika watu waliokufa!" # Kwanini mnamtafuta Hapa inamaanisha wengi, inaongelea juu ya wanawake waliokuja.