# Alipoamka kutoka katika maombi yake Tafrisi mbadala: "Wakati Yesu alipoamka baada ya kuomba" au "Baada ya kuomba, Yesu aliamka na" # akawakuta wamelala kwa sababu ya huzuni nyingi "aliwaona kwamba walikuwa wamelala kwa sababu walikuwa na huzuni sana" # Kwanini mnalala? Inaweza kumaanisha 1) "Nashangazwa kwamba mnalala sasa" au 2) "Hampaswi kuwa mmelala sasa hivi!" # kwamba msiingie majaribuni "msijaribiwe" au "hakuna kitu cha kuwajaribu na kuwafanya mtende dhambi"