# ambayo yameandikwa kwa ajili yangu Tafsiri mbadala:"ambayo nabii ameandika kuhusu mimi katika maandiko" # lazima yatimilike Mitume wangelimuelewa Mungu kwamba angesababisha yote yaliyoandikwa kwenye maandiko kutokea. Tafsiri mbadala: "Mungu atatimiliza" au "Mungu atayafanya yatokee." # alichukuliwa kama mtu ambaye anavunja torati Hapa Yesu ananukuu maandiko. Tafsiri mbadala: " watu walimchukulia kama mtu ambaye hafuati au hana sheria." # Mvunja sheria "Wale wanaovunja sheria" au "waharifu" # Kwa sababu kile kilichotabiriwa kwa ajili yangu Inaweza kumaanisha 1) "Yale ambayo mtume ametabiri kuhusu mimi yako tayari kutokea" au 2) "Kwa kuwa maisha yangu yanafikia ukingoni." # wakasema Hii inamaanisha angalau wawili wa mitume wa Yesu. # yatosha Inaweza kumaanisha 1) "Hizo panga zinatosha" au 2) "Hiyo inatosha kuiongelea." Yesu aliposema wanatakiwa kununua panga, alikuwa hasa akiwaambia kuhusu hatari ambazo wote watazikabili. Inawezekana si kwamba aliwataka wanunue panga na wapigane.