# Taarifa ya kijumla: Yesu anaongea moja kwa moja na Simoni. # Simon, Simon Yesu alilisema jina lake mara mbili kuonyesha kwamba kile ambacho alikuwa akiseme kwake kilikuwa cha muhimu sana. # awapate, ili awapepete Neno "awa" linaonyesha mitume wote. # awapepete kama ngano Hii inamaanisha kwamba Shetani alitaka kuwajaribu mitume ili kupata makosa. # Lakini nimekuombea Hapa inamaanisha amemuombea kipekee kabisa SImoni. # kwamba imani yako isishindwe "kwamba utaendelea kuwa na imani" au "utaendelea kunitegemea mimi" # Baada ya kuwa umerudi tena "Baada ya kuanza kunifuata tena" au "Baada ya kuanza kunitumikia mimi tena" # ndugu zako Hii inamaanisha wanafunzi wengine wa Yesu. Tafsiri mbadala: "Waamini wenzako" au "mitume wengine."