# wakati wa mchana alikuwa akifundisha "wakati wa mchana angeweza kufundisha." Mistari inayofuata kuhusu vitu ambavyo Yesu na watu walifanya kila siku katika wiki kabla hajafa. # hekaluni Tafsiri mbadala: "katika hekalu" au "kwenye uwanja wa ndani wa hekalu" # usiku alitoka nje "usiku angeliweza kwenda nje ya mji" au "alikwenda nje kila usiku" # Watu wote Tafsiri mbadala: "idadi ya watu wengi sana" au "karibu kila mmoja" # walimuijia asubuhi na mapema "wangekuja asubuhi na mapema" au "walikuja mapema sana kila asubuhi" # kumsikiliza "kumsikiliza akifundisha"