# Mwana wa Adamu Yesu anarejea kwake mwenyewe # akija mawinguni Tafsiri mbadala: "akija chini katika mawingu" # katika nguvu na utukufu mkuu Hapa "nguvu" inawezekana inarejea katika mamlaka yake kuuhukumu ulimwengu. Hapa "utukufu" unaweza kurejea mwanga angavu. Mungu wakati mwingine anaonyesha ukuu wake na mwanga angavu sana. Tafsiri mbadala: "a nguvu na utukufu" au "atakuwa na wa nguvu na wa utukufu sana." # simameni Wakati mwingine watu wanapoogopa, hujiinamisha chini ili kuepuka kuonekana au kuumizwa. Wakati wanapokuwa hawaogopi tena, wananyanyuka. Tafsiri mbadala: "simameni na ujasiri." # inueni vichwa vyenu Tafsiri mbadala: "tazameni juu." Kwa kutazama juu, wataweza kumuona mwokozi akija kwao. # kwa sababu ukombozi wenu unasogea karibu Tafsiri mbadala: "kwa sababu mkombozi wenu anakuja kwenu" au "kwa sababu Mungu mara atawaokoa"