# Kwahiyo "Kwa sababu ya hili." Yesu anatumia neno hili hapa kurejea kwenye kila kitu alichokisema. # amueni mioyoni mwenu Tafsiri mbadala: "zingatieni akilini mwenu" au "amua kiuthabiti" # kutoandaa utetezi wenu "kutokufikiri nini ambacho mtasema ili kujitetea kinyume cha mashitaka yao" # nitawapa maneno na hekima "Nitawaambia maneno gani ya hekima ya kusema" # maneno na hekima Tafsiri mbadala: "maneno ya hekima" # ambayo adui zenu wote hawataweza kuipinga au kuikataa kwamba ni uongo. Hii inaweza kutafsiriwa kama sentensi mpya. Tafsiri mbadala: "Adui zenu hawataweza kubishana na ninyi au kusema kwamba hamko sahihi" au "Adui zenu lazima wakubali kwamba mko sahihi."