# mambo haya Hii inamaanisha mambo mabaya ya kutisha ambayo Yesu alisema yatatukia. # wataweka mikono yao juu yenu Tafsiri mbadala: "watawakamata" au "watawashika" # wata... "watu wata.." au "adui wata..." # yenu Yesu alikuwa akiongea na wanafunzi wake. # kuwapeleka kwenye masinagogi "kuwatoa ninyi kwa viongozi wa masinagogi." Viongozi wa masinagogi wangewakataza Wayahudi wengine wote kuingiliana na wanafunzi kwa sababu wanamfuata Yesu. # na magereza "na kuwapeleka ninyi magerezani" au "na kuwaweka ninyi magerezani" # kwa sababu ya jina langu Tafsiri mbadala: "kwa sababu yangu" au "kwa sababu mnanifuata mimi" # kwa ushuhuda wenu "kwa ninyi kuwaambia wao ushuhuda wenu kunihusu mimi"