# mjane mmoja maskini Hii ni namna ya kutambulisha mtu mpya katika hadithi # zawadi "zawadi za fedha" # hazina "sanduku la makusanyo" au "sanduku la fedha". Hili lilikuwa moja ya masanduku pale hekaluni ambapo watu huweka fedha kama zawadi kwa Mungu. # senti mbili "sarafu mbili ndogo" au "sarafu za shaba ndogo sana". Hizi zilikuwa ni sarafu zenye thamani ndogo sana ambazo watu walizitumia siku hizo. # Nawaambieni Yesu alikuwa akiongea na wanafunzi wake. # wametoa hizi zawadi kutoka katika vingi walivyonavyo Tafsiri mbadala:"kuwa na fedha nyingi na kutoa baadhi ya hizo" # katika umaskini wake, ametoa zote Tafsiri mbadala:"alikuwa na vichache sana, na bado aliweka vyote"