# Maelezo ya Jumla Hii ni sehemu nyingine ya simulizi. Yesu anakaribia Yerusalemu. # Ikawa Aya hii imetumika kuonyesha mwanzo wa simulizi mpya. Kama lungha yako ina njia nyingine ya kusema hivi unaweza ukatumia hivyo. # Alipofika karibu Neno "yeye" linamaanisha Yesu. Wanafunzi wake walisafiri pamoja naye. # Bethfage Bethfage kilikuwa kijiji kwenye mlima wa Mizeituni, ambayo imepita katikati ya bonde la Kidron toka Yerusalemu. # Mlima ulioitwa Mizeituni "Mlima ulioitwa Mlima wa Mizeituni" au Mlima ulioitwa "mlima wa mti wa Mizeituni" # Mwanapunda "Punda mdogo" au "myama mdogo wa kumuendesha" # Ambaye hajapandwa bado "ambae hamna mtu aliyemtumia"