# Hivyo Neno hili linaweka alama ya tukio limetokea kwa sababu kitu fulani kilitokea kwanza. Kwa hivyo makutano walimwambia kipofu kuwa Yesu anapita. # Akalia kwa sauti "akaita kwa sauti" au "akapiga kelele" # Mwana wa Daudi Yesu alikuwa uzao wa Daudi, Mfalme muhimu kwa Israeli. # Nihurumie "nionee huruma" au "nihurumie" # Wale "watu" # Anyamaze "awe kimya" au "asipige kelele" # Akazidi kulia kwa sauti Hii inaweza kumaanisha alilia kwa sauti zaidi au alilia zaidi kwa kusisitiza.