# Taarifa ya jumla Hii ni sehemu nyingine ya simulizi. Yesu anamponya kipofu alipokuwa anakaribia Yeriko. Mistari hii inatupa historia kuhusu simulizi hii. # Ikawa Neno hili linatumika kuonyesha mwanzo wa simulizi mpya. # Alipokaribia "Alipokuwa karibu" # Mtu mmoja kipofu alikuwa ameketi "kulikuwa na mtu kipofu ameketi" Hapa "mmoja" inaonyesha kuwa mtu huyu alikuwa wa muhimu katika simulizi hii lakini Luka hakutaja jina lale. # Akiomba, na akasikia "Aliomba. aliposikia" # Wakamwambia "Makutano wakamwambia kipofu" # Yesu wa Nazareti Yeso toka mji wa Nazareti uliopo Galilaya. # Anapiata "Alikuwa akimpita"