# Sasa kulikuwa na mjane Yesu alitumia neno hili kumtambulisha mtu mwingine kwenye simulizi. # Mjane Ni mwanamke ambaye mume wake amekufa. Watu waliomsikiliza Yesu watafikiri kuwa ni mtu ambaye hamna mtu wa kumlinda kutoka kwa wale wanaotaka kumuumiza. # Alimwendea mara nyingi Neno "yeye" linamaanisha hakimu. # Nisaidie kupata haki dhidi "waadhibu" au "nisaidie" # Mpinzani wangu "adui yangu" au "mtu anayejaribu kuniumiza." Huyu ni mpinzani katika mabo ya sheria. Hipo wazi kuwa mwanamke anamshitaki yule mtu au yule mtu anamshitaki mwanamke. # Kumwogopa Mungu "ogopa Mungu" # Mtu Hii inamaanisha "watu" kwa ujumla. # Ananisababishia matatizo "Ananisumbua" # Asinichoshe "asije akanisumbua" # Kwa kunijia mara kwa mara "kwa kuja kwangu mara kwa mara"