# Habari kwa ujumla: Hii ni sehemu ya pili ya hadithi. Hatujui ambapo hili limetokea; ni siku moja wakati Yesu akizungumza na Mafarisayo. # Alipoulizwa na mafarisayo ufalme wa Mungu utakuja lini, Yesu akawajibu akisema, Hii ​​inaweza semwa kama: "wakamuuliza 'Lini Utawala wa Mungu utakuja?" # Alipoulizwa na Mafarisayo Huu ni mwanzo wa sehemu mpya ya hadithi. Baadhi ya tafsiri huanza kwa "Siku moja" au "Mara." # Ufalme wa Mungu sio kitu ambacho kinaweza kuonekana Hii inaweza kusemwa: "Ufalme wa Mungu si kitu ambacho unaweza kuona kwa macho yako" au "Ingawa unanngalia Ufalme wa Mungu, huwezi kuuona" # Utawala wa Mungu uko kati yenu "Utawala wa Mungu uko hapa" au "Mungu tayari ameanza kutawala kati yenu"