# Habari kwa ujumla: Hii ni sehemu ya pili ya hadithi. Yesu anaponya watu 10 wa ukoma. Mstari wa 11 na 12 unatoa taarifa za msingi na mazingira ya hadithi. # Ikawa kwamba maneno haya yametumika hapa kuonyesha mwanzo wa sehemu mpya ya hadithi. Kama lugha yako ina njia kwa ajili ya kufanya hii, unaweza kufikiria kutumia hapa. # na walipokua njiani kuelekea Yerusalemu "kama Yesu na wanafunzi walipokuwa wakisafiri kwenda Yerusalemu" # huko alikutana na watu kumi wenye ukoma Hii inaweza semwa kama. "watu kumi wenye ukoma walikutana naye" au "watu kumi waliokuwa na ukoma walikutana naye" # wakapaza sauti zao kauli hii ina maana kusema kwa sauti kubwa. "wakamwita kwa sauti kubwa" au "wao kuita kwa sauti" # Bwana neno lililotafsiriwa hapa kama "Bwana" siyo neno la kawaida kwa "Bwana." Hii moja inahusu mtu ambaye ana mamlaka, na si kwa mtu ambaye anamiliki mtu mwingine. # utuhurumie Walikuwa hasa wanaomba kuponywa. "tafadhali tuonyeshe huruma na utuponye" # alipokuwa akisafiri kwenda Yerusalemu "kama Yesu na wanafunzi walikuwa wakisafiri kwenda Yerusalemu" # kijiji kimoja maneno haya haya elezei hicho kijiji. # Nao wakasimama mbali mbali na yeye Hii ilikuwa ishara ya heshima , kwa sababu wenye ukoma hawakuruhusiwa kukaribia watu wengine.