# Kauli inayounganisha Katika mstari wa 42, Yesu aliendelea kuelezea mfano # Kauli ya jumla Katika mstari wa 41, kuna katizo katika kuelezea mfano kwani Petro alimuuliza Yesu swali kuhusu mfano. # Ni nani...kwa wakati mwafaka Yesu alitumia swali kufundisha watu. Yesu hakujibu swali la Petro moja kwa moja, lakini alitegemea wale wanaotaka kuwa watumwa waaminifu kuwa mfano huo inawahusu wao. " Nimesema kwa kila mmoja ambaye ..kwa wakati mwafaka. # Mtumwa mwaminifu na mwenye hekima Yesu alielezea mfano mwingine wa jinsi watumishi wanavyotakiwa kuwa waaminifu wakati wanamngoja bwana wao arudi. # ambaye bwana wake atamuweka juu ya watumishi wengine "ambaye bwana wake atamuweka kuwa mtawala wa wengine" # Amebarikiwa mtumishi yule "Itakuwa heri kwa mtumishi yule" # ambaye bwana wake akija atamkuta akifanya "kama bwana wake akirudi atamkuta akifanya kazi hiyo"