# Kauli inayounganisha Yesu aliendelea kuwafundisha wanafunzi wake mbele ya umati. # Kwahiyo "kwasababu hiyo" au " kwasababu ya mafundisho ya hadihi hii" # Nawaambia "Nataka niwaambie kitu muhimu"au "Inabidi msikilize kwa umakini juu ya hili" # juu ya maisha yenu-ya kuwa mtakula nini "kuhusu maisha yenu na nini mtakula" au " kuhusu kuwa na chakula cha kutosha ili muweze kuishi" # juu ya miili yenu -ya kuwa mtavaa nini "kuhusu miili yenu na nini mtavaa" au " kuhusu kuwa na nguo za kutosha za kuvisha miili yenu"