# Kwasababu hiyo Hii inarejea sentensi iliyofuata, Mungu atawatuma manabii wengi ili kuonesha kuwa kizazi hiki kitawauwa, kama walivyofanya baba zao. # Hekima ya Mungu inasema "Mungu kwa hekima yake alisema" au "Mungu alisema kwa hekima" # Nitawatumia manabii na mitume "Nitawatumia manabii na mitume watu wangu" # watawatesa na kuwauwa baadhi yao "watu wangu watawatesa na kuwauwa baadhi ya manabii na mitume" # Kizazi hiki, kitawajibika na damu iliyomwagwa ya manabi wote. Damu iliyomwagwa inamaanisha mauwaji ya manabii. "Kwa hiyo Mungu atawajibisha kizazi hiki kwa kifo cha manabii wote ambao watu wamewauwa" # Zakaria Huyu ni kuhani wakati wa Agano la kale aliyewakemea watu wa israeli kwa habari ya usinzi. Huyu siye Baba wa Yohana Mbatizaji. # ambaye ameuwawa "ambaye watu walimuuwa"