# mahali pasipo maji "Hii inamaanisha "sehemu ya ukiwa", mahali ambapo roho mbaya hurandaranda . # akikosa "kama roho hakupata sehemu ya kupumzika" # nyumba yangu nilikotokea Hii inamaanisha mtu yule ambaye alikuwa anakaa kwake. "mtu ambaye nilikuwa nikikaa kwake" # na kukuta nyumba imefagiliwa na imekaa vizuri "akaikuta mtu alifagia nyumba na kuwa safi na kuweka kila kitu mahali pake " au " kumkuta mtu kama nyumba iliyosafishwa na kupangiliwa vizuri" # imefagiliwa "tupu" Mfano huu inamaanisha hali ambayo mtu hakujazwa Roho wa Mungu baada ya mapepo kuondoka.