# Kila kitu kimekabithiwa kwangu kutoka kwa Baba yangu AT: " Baba yangu amekabidhi kila kitu kwangu". # Baba... Mwana. Hivi ni vichwa vikuu vya muhimu vinavyoelezea uhusiano kati ya Mungu na Yesu. # Mwana Yesu alikuwa akijizungumzia yeye katika nafasi ya tatu. # afahamuye Mwana ni nani Neno ambalo limetafasiriwa kama "Afahamuye" linamaanisha kujua kutokana na kumwelewa mtu. Mungu Baba anamjua Yesu kwa namna hiyo. # Ila Baba Hii inamaanisha ni Baba peke yake anajua Mwana ni nani. # na yeyote ambaye mwana anatamani kujifunua kwake AT: "na watu watajua Baba ni nani endapo Mwana atataka kuwadhihirishia Baba kwao".