# Ndipo akamwambia "ndipo akamwabia mwanamke" (UDB) # Dhambi zako zimesamehewa "umesamehewa." Hii inaweza ikasemwa katika kauli tendaji NI: "Nasamehe dhambi zako" # kaa pamoja "kaa pamoja kuzunguka meza" au "kula pamoja" # Nani huyo hata anasamehe dhambi Viongizi wa dini walijua kwamba Mungu tu anayesamehe dhambi, na hawakuamini kwamba Yesu alikuwa Mungu, Swali hili huenda lilikusudiwa kuwa tuhuma. NI: "Huyu mtu anafikiri kuwa yeye ni nani?" Ni Mungu pekee anaye samehe dhambi!" au "Kwanini huyu mtu anajifanya kuwa Mungu awezaye kusamehe dhambi?" # Imani yako imekuponya wewe "Kwa sababu ya imani, umeokoka" "imani" inaweza ikatazamwa kama kitendo. NI: "kwa sababu umeamini, umeokoka" # Nenda katika amani Hii ni namna ya kusema kwaheri wakati huohuo unatoa baraka. NI: "Unapokwenda, usiwe na wasi wasi kabisa" au "Mungu akupe amani unapoenda"