# Taarifa kwa Ujumla: Yesu analinganisha mawazo ya mtu kwa hazina nzura au mbaya. Mawazo mazuri ya mtu mzuri yanasababisha matendo mazuri. Mawazo maovu ya mtu mwovu husababisha matendo mabaya. # Mtu mwema Neno "mwema" hapa linahusu mwenye haki au maadili mema. # mtu mwema Neno "mtu" linarejea kwa mtu, mwanaume au mwanamke. NI: "mtu mwema" # Hazina njema ya moyo wake "vitu vizuri hutunza moyoni mwake" au "vitu vizuri huvithamini" # huzaa kilicho kizuri Kutoa kilicho kizuri ni sitiari kwa kufanya mema. NI: "kufanya kilicho kizuri" # hazina mbaya ya moyo wake "mambo mabaya anayotunza moyoni mwake" au "mambo mabaya anayothamini" # katika utajiri wa moyo wake mdomo huzungumza Kirai "kinywa chake" kinawakilisha yeye kutumian mkinywa chake. NI: "anachofikiri moyoni mwake kinaathiri anachosema kwa mdomo wake" au anachokithamini moyoni mwake huamua kinachosemwa na kinywa.