# Sentensi Unganishi: Yesu alipoondoka nyumbani, anamwita Lawi, Myahudi mtoza ushuru amfuate. Lawi anaandaa mlo kwaajili ya Yesu uliowakera mafarisayo na waandishi. # Baada ya mambo hayo kutokea Kirai "vitu hivi" kinamaanisha kilichotokea kwenye mistari iliyopita. Ishara hii ni tukio jipya. # akamwona mtoza ushuru "akamwangalia mtoza ushuru kwa umakini "au" alimwangalia mtoza ushuru kwa uangalifu" # Nifuate Kufuata mtu ilikuwa ni kauli imaanishayo kuwa mwanafunzi. NI: "Kuwa mwanafunzi wangu "au" njoo, nifuate kama mwalimu wako" # Acha vyote nyuma "akaacha kazi yake kama mtoza ushuru"