# Sentensi Unganishi: Ingawa watu walitaka Yesu abaki Kapernaumu, anakwenda kuhubiri kwenye masinagogi mengine Uyahudi. # ilipofika mapambazuko "wakati wa jua kuchomoza" # mahali palipo jitenga "mahali pa pekee" au "mahali pasipokuwa na watu" # kwa miji mingi mingine "kwa watu katika miji mingine mingi" # hii ni sababu nilikuwa nimetumwa hapa Hii inaweza ikawekwa kwenye kauli tendaji, NI: "hii ni sababu Mungu alinituma hapa mimi" # Uyahudi Tangu Yesu awe Galilaya, neno "Uyahudi" hapa huenda linarejea kwenye ukanda wote ambako Wayahudi waliishi wakati huo, NI: "ambapo waliishi Wayahudi"