# Sentensi Unganishi Yesu bado yuko Kapernaumu, lakini sasa yuko katika nyumba ya Simoni, alipomponya mama mkwe wa Simoni na watu wengi. # Ndipo Yesu akaondoka Hii inaanzisha tukio jipya # Mama mkwe wa Simoni Mkwe - "mama yake mke wa Simoni" # Alikuwa anaumwa Hii ni nahau inayomaanisha "alikuwa anaugua" # homa kali "mwili wake ulikuwa na joto kali" # kusihi badala yake Maana yake walimwomba Yesu amponye homa yake. Hii inaweza kusemwa wazi. NI: "kumwomba Yesu amponye homa" # Hivyo alisimama Neno "Hivyo" linaweka wazi kwamba alifanya hivi kwa sababu watu walimsihi badala ya mama mkwe wa Simoni. # alisimama kwake "alikwenda kwake na aliegama kwake" # liikemea homa "alisema kwa kuikaripia homa" au "aliamuru homa kumwacha" UDB. Itakuwa ni msaada kusema wazi alichoiambia homa kufanya. NI: "aliiamuru ngozi kupoa" "aliuamuru ugonjwa kumwacha" # alianza kuwahudumia Hapa hii inamaana alianza kuandaa chakula kwaajili ya Yesu na watu wengine ndani ya nyumba.