# Sentensi Unganishi: Yesu alirudi Galilaya, akifundisha katika Sinagogi, na anawaambia watu pale kwamba yeye anatimiza maandiko ya Isaya nabii. # Ndipo Yesu alirudi Hii inaanza simulizi jipya katika habari. # katika nguvu ya Roho "na Roho alikuwa anampa yeye nguvu." Mungu alikuwa pamoja na Yesu kwa namna maalumu, anamwezesha yeye kufanya vitu ambayo kawaida watu wasingeviweza. # habari kumhusu yeye zikaenea Wale waliomsikia Yesu waliwaambia watu wengine kuhusu yeye, na ndipo wale watu wengine waliwaambia hata zaidi kuhusu yeye. Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. NI: "watu wakaeneza habari kuhusu Yesu" au "watu waliwaambia watu wengine kuhusu Yesu" au "maarifa kumhusu yeye yalikuwa yakipita kutoka kwa mtu kwenda mtu mwingine" # kupitia katika eneo lote linalozunguka ukanda Hii inarejea kwenye maeneo au mahali karibu na Galilaya. # likuwa anasifiwa na wote "kila mmoja alisema mambo makuu kuhusu yeye" au "watu wote walimsema vizuri "