# Lakini Yesu alijibu ... imeandikwa Utofauti huu unamaanisha kwamba Yesu alikataa kufanya kile alichoambiwa na Ibilisi. Itakuwa msaada kusema hiki wazi kwa hadhara yako. NI: "Lakini alijibu, 'Hapana, sitakuabudu wewe, kwa sababu imeandikwa" (UDB) # alijibu na akamwabia "akamjibu" au "alimjibu" # Imeandikwa Hii inaweza ikasemwa katika kauli tendaji. NI: "Musa ameandika katika maandiko" # Utamwabudu Bwana Mungu wako Yesu alikuwa ananukuu amri kutoka kwenye maandiko kusema kwanini hataweza kumwabudu Ibilisi. # Wewe Hii inarejea kwa watu katika Agano la Kale waliopokea amri ya Mungu. Unawea kutumia kauli ya umoja 'wewe' sababu kila mtu ilikuwa atiii, au ungetumia kauli ya wingi "ninyi" sababu watu walipaswa kuitii. # yeye Neno "yeye" anarejea kwa Mungu.