# Maelezo kwa Ujumla Mwandishi, Luka, kanukuu mstari kutoka nabii Isaya tokana na Yohana Mbatizaji. # Kama ilivyoandikwa...nabii Misitari 4-6 ni nukuu kutoka Isaya. Ingeweza kuelezewa katika hali ya kutenda. AT: "Hii ilitokea kama Isaya alivyokuwa ameandika katika kitabu chake" au "Yohana aliyatimiza maneno ambayo Isaya alikuwa ameyaandika katika kitabu chake." # Sauti ya mtu inapazwa nyikani Hii inaweza kudhihirishwa kama sentensi. NI: "Sauti ya mmoja inapazwa ikisikika katika nyika" au "Wanasikia sauti ya mtu fulani inapazwa katika nyika" # Itengenezeni njia ya Bwana ... tengeneza mapito kwa unyoofu Kauli hizi mbili kimsingi ni kitu kile kile. # Tayarisha njia ya Bwana "Andaa njia kwaajili ya Bwana." Kufanya hivi kunawakilisha kujiandaa kusikia ujumbe wa Bwana anapokuja. Watu hufanya hivi kwa kutubu dhambi zao. NI: "Andaa kusikia ujumbe wa Bwana anapokuja" au "Tubu na uwe tayari kwaajili ya ujio wa Bwana" # njia "pa kupita" au "barabara"