# Nabii mke jina lake Ana pia alikuwa pale Hii inatambulisha mhusika mpya katika simulizi. # Fanueli "Fanueli" ni jina la mwanaume. # miaka saba "miaka 7 " # baada ubikra wake "baada ya kuolewa naye" # mjane kwa miaka themanini na minne miaka minne - Maana zinazowezekana 1) kawa mjane kwa miaka 84 au 2) alikuwa mjane na alikuwa na umri wa miaka 84. # hakuondoka hekaluni Hii huenda ni maana iliyokuzwa kwamba alitumia muda mwingi katika hekalu hii ilionekana kama kwamba hakuondoka pale. NI: "kila mara alikuwa hekaluni" au "daima alikuwa hekaluni." # akifunga na kuomba "kujinyima chakula na maombi" # akawajia karibu yao "kuwafuata" au "alikwenda kwa Mariamu na Yusufu" # wokovu wa Yerusalemu Hapa neno "wokovu" lilitumika kurejea kwa mtu ambaye angetenda. NI: yule ambaye angeokoa Yerusalemu" au "mtu ambaye angeleta baraka za Mungu na fadhila tena kwa Yerusalemu."