# Ikawa kauli hii ilitumika kuonesha kubadili kwa masimulizi kwenda kwenye ambacho wachungaji walifanya baada ya malaika kuondoka. # kutoka kwao "kutoka kwa wachungaji" # Baina ya mtu na mtu "kwa mmoja na mwingine" # ngoja nasi ... kwetu Tangu wachungaji walikuwa wanazungumza mmoja na mwingine, lugha ambayo inamtindo wa kuhusisha kwa "sisi" na "nasi" tumia mtindo wa kuhusisha hapa. # ngoja nasi "nasi tuta" # jambo hili ambalo limetokea Hii inarejea kuzaliwa kwa mtoto, na siyo kuonekana kwa malaika. # kalala katika kihori cha kulishia Hii ilikuwa aina fulani ya boksi au kitu ambacho watu waliweka nyasi kavu au chakula kwaajili ya wanyama kula. Angalia jinsi ilivyotafsiriwa katika 2:6.