# Maelezo kwa ujumla: Hii inatuambia kwa kifupi kuhusu miaka ya Yohana kuongezeka. # Sasa Neno hili linatumika hapa kuonesha kituo kwenye mfululizo wa habari kuu. Luka anahama kwa haraka kutoka kuzaliwa kwa Yohana kwenda kwenye huduma yake. # kuwa na nguvu katika roho "kukomaa kiroho" au "kuimarisha uhusiano na Mungu" # alikuwa katika mwitu "aliishi katika mwitu." Luka hasemi katika umri gani Yohana alianza kuishi mwituni. # mpaka Hii siyo lazima kuonesha hoja ya kumalizia. Yohana anaendelea kuishi katika pori hata baada ya kuanza kuhubiri hadharani. # siku ya kujitokeza kwake "alipoanza kuhubiri hadharani" # siku Hii ilitumika hapa katika dhana ya jumla ya "wakati" au "fursa"