# kuonesha rehema "kuwa na huruma kwa" au "kutenda kutokana na rehema yake kwao" # kumbuka Hapa neno "kumbuka" linamaana kuendelea kujitoa au kukamilisha kitu fulani. # agano lake takatifu ... kiapo ambacho alikisema Kauli hizi mbili zinarejea kwenye kitu kile kile. Zimerudiwa kuonesha kujali kwa Mungu juu ya ahadi kwa Abrahamu. # kutoa idhini kwetu "kufanya iwezekane kwaajili yetu" # kwamba sisi, tumekombolewa ... tumtumikie yeye bila hofu Inaweza ikasaidia kubadili mtindo wa kauli hizi. NI: "kwmba tungelimtumikia yeye bila bila hofu baada sisi kuokolewa kutoka katika nguvu za adui wetu." # kutoka katika mkono wa adui zetu "mkono" inarejea kudhibiti au nguvu ya mtu. Hii inaweza kusemwa wazi. NI: "kutoka katika udhibiti wa adui zetu." # bila hofu Hii inarejerea nyuma kwenye hofu ya adui zao. NI: "bila kuwaogopa adui zetu" # katika utakatifu na haki Hizi zinaweza kudhihirishwa kama matendo. NI: "kuishi katika njia safi na kutenda haki" # mbele yake Nahau hii ambayo inamaanisha "katika uwepo wake"