# Baada ya siku hizi Kauli "siku hizi" inarejea wakati Zakaria alikuwa anatumika hekaluni. Hii inawezekana kulisema hili kwa uwazi. NI: "Baada ya Zakaria kurudi nyumbani tokea kwenye huduma hekaluni." # mke wake "mke wa Zakaria" # alijitenga mwenyewe "hakuondoka nyumbani kwake" au "alibaki peke yake ndani" # Hiki ndicho alichokifanya Bwana kwaajili yangu Kauli hii inarejea ukweli kwamba Bwana alimruhusu apate ujauzito. # hiki ndicho Hili ni tamko zuri la mshangao. Yeye alikuwa na furaha sana kwa kile alichokitenda Bwana kwaajili yake. # aliniangalia mimi kwa upendeleo "Kuangalia" ni nahau ambayo inamaanisha "kutendea" au "kushughulikia." NI: "tazama kwa wema" au "alinihurumia" # aibu yangu Hii inarejea kwenye aibu aliyoihisi kwa sababu alikuwa hawezi kuwa na watoto.