# Kwa hiyo Yahweh akazungumza na Musa na akasema, "Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, 'Yeye atoaye Hii ina nukuu ndani ya nukuu. Nukuu ya moja kwa moja yaweza kutamkwa kama nukuu taarifa yenyekutajwa. : Kisha Yahweh akazungumza na Musa na akamwambia awaambie watu wa Israeli kwamba: 'Yeye atoaye" # Mikono yake mwenyewe lazima iilete hiyo sadaka ifanywayo kwa Yahweh kwa moto Kile kirai "ifanywayo kwa moto" yaweza kutamkwa katika mtindo wa utendaji. : "Yeye mwenyewe analazimika kuileta sadaka anayopanga kuiteketeza kama dhabihu kwa Yahweh" # Mikono yake mwenyewe "Mikono" humwakilisha mtu mzima. : "yeye mwenyewe anapaswa kuileta" # kidari Sehemu ya mbele ya mwili wa mnyama iliyoko chini ya shingo # ili kwamba kidari kiweze kutikiswa kuwa sadaka ya kutikiswa mbele za Yahweh. Hii yaweza kufasiriwa katika mtindo wa utendaji. : "ili kwamba kuhani aweze kuiwasilisha kwa Yahweh kama sadaka ya kutikiswa" # kiweze kutikiswa kuwa sadaka ya kutikiswa mbele za Yahweh. Kuiinua juu sadaka ni mfano wa ishara unaoonyesha kwamba mtu anaiweka wakfu dhabihu kwa Yahweh.