# Taarifa kwa ujumla Yahweh anaendelea kumwambia Musa kiwapasacho watu kutenda ili matoleo yatakubalika kwa kwake. # wataweka moto juu ya madhabahu na kuweka kuni ili kuuchochea huo moto Hili laweza kumaanisha kwamba makuhani mkaa wa moto juu ya madhabahu, kisha wakaweka kuni juu ya mkaa. : wataweka kunu juu ya madhabahu na kuwasha moto" # kuuchochea huo moto Hii ni nahau inayomaanisha kuendelea kuweka kuni kwenye moto. Moto juu ya madhabahu nilazima uendelee kuwaka bila kuzimika # Lakini matumbo yake na miguu ataiosha kwa maji Mtu huyo angefanya hivi kabla hajavitoa vipande kwa makuhani waviweke juu moto. U naweza kutamka hivi mwishoni mwa 1:5 # Mtumbo Ni hilo tumbo na utumbo # naye ataiosha Hapa neno "naye" humaanisha anayetoa hiyo sadaka. # nayo italeta harufu ya kupendeza kwangu Yahweh akiwa amependezwa na utoaji dhabihu wa dhati wa aabuduye unamezungumziwa kana kwamba Yahweh alikuwa amependezwa na harufu nzuri ya dhabihu. # sadaka iliyofanywa kwangu kwa moto. Yahweh anamwambia Musa kwamba ni lazima matoleo yawe yanachomwa kwa moto. Hili laweza kutamkwa katika muundo tendaji. : "sadaka ya kuteketezwa kwangu"