# Usiogope; usivunjike moyo Vifungu hivi viwili vya maneno kimsingi vinamaanisha kitu kimoja. Yahweh ameviunganisha pamoja kutia mkazo kwamba hakuna sababu ya kuogopa. # nimemtia mkononi mwako mfalme wa Ai... na nchi yake Kuwatia katika mkono wa Israeli ina maana ya kuwapa waisraeli ushindi na kuwatawala. "Nimewapeni ushindi dhidi ya mfalme wa Ai na watu wake, na nimewapeni utawala juu ya mji wake na nchi yake." # Nimewapeni Mungu anaongelea juu ya ahadi alizoahidi kufanya kana kwamba alikuwa ameshakifanya, kwasababu atalifanya kwa uhakika. "NItawapa kwa uhakika" # mfalme wake Neno 'wake' inarejelea mji wa Ai.