# Sentensi kiunganishi Yoshua anaendelea kuongea na watu wa israeli. # Mji pamoja na vitu vyote ndani yake vitatengwa kwa Yahweh kwa ajili ya uharibifu. Sentensi hii yaweza kuelezwa kwa kauli tendaji: "Ni lazima kuzitenga kwa Yahweh mji na kila kitu ndani yake kwa ajili ya kuharibiwa" # iweni waangalifu juu ya kuchukua vitu Kuwa mwangalifu kunaongelewa kana kwamba wao ni walinzi wenyewe. "Iweni waangalifu msivichukue vitu" # mtaleta matatizo katika kambi Kufanya kitu fulani kinachofanya mambo mabayaa kutokea katika mji kunasemwa kama kuleta matatizo juu yake. # Hazina ya Yahweh Mkusanyiko wa vitu vilivyotengwa kwa ajili ya kumwabudia Yahweh.