# Maelezo ya jumla Yoshua anawaambia Waisraeli maana ya fungu la mawe kumi na mawili. # Maji ya Yordani yalitengwa mbele ya sanduku la Yahweh Sentesi hii inaweza kuelezwa katika kauli tendaji: "Yahweh aliyatenga maji ya Yordani mbele ya sanduku la agano lake" # Maji ya Yordani Mto Yordani # yalitengwa mbele ya sanduku la Yahweh Mto Yordani ulizuiliwa na Mungu ili usitiririke kuelekea sanduku la Agano ambalo lilikuwa limebebwa na makuhani. # maji ya Yordani yalisimamishwa Maji yaliyotiririka katika Mto Yordani yalikoma mbele ya sanduku ili kwamba kila mtu pamoja na agano lenyewe lisafiri katika nchi kavu.