# Maelezo ya jumla Rahabu anaendelea kuongea na wapelelezi wa Kiisraeli. # Bahari ya mianzi Hili ni jina jingine la Bahari Nyekundu # Sihoni na Ogu Haya ni majina ya wafalme wa Waamori # mioyo yetu iliyeyuka na hapakuwa na ujasiri wowote uliosalia Virai hivi vya maneno vina maana sawa, yameunguanishwa ili kuonesha mkazo. Maneno "mioyo yetu ikayeyuka" yanalinganisha mioyo ya watu waoga na kuyeyuka kwa barafu na kutiririka.