# Maelezo ya jumla Yahweh anaendelea kumtia changamoto Ayubu # Je umempa farasi ... panzi? Yahweh anatumia maswali haya kutia mkazo kwamba ni yeye ndiye huyafanya mambo haya ambayo Ayubu hayawezi. # umeivika shingo yake Neno 'kuvika" ni njia ya kuelezea jinsi ambavyo Yahweh alivyoifanya shingo ya farasi. # manyoya yake ni nywele ndefu ambazo hushuka chini kutoka katika shingo ya farasi na hutisika wakati farasi anapoondoka. # nzige ni aina kubwa ya panzi ambayo yaweza kuruka kwenda mbali na kwa haraka sana. # mlio ni sauti kubwa ambayo farasi huitoa katika pua zao.