# Maelezo ya jumla Yahweh anaendelea kumtia changamoto Ayubu # je nyati...bonde kwa ajili yako? Yahweh anatumia maswali haya ili kutia mkazo kwamba Ayubu hawezi kuwatawala nyati. # Nyati Maana zinazowezekana ni 1) "ng'ombe wa porini" 2)"swala" aina fulani ya swala anayeonekana kama ng'ombe dume. # kuwa na furaha "kuridhia" # atakubali kukaa katika zizi lako "kukaa karibu na zizi wakati wote wa usiku" # hori/zizi Katika mazingira ya Israeli, hiki kilikuwa ni chombo cha kulishia wanyama # mtaro Ni mfereji mrefu uliotengenezwa katika sehemu chafu kwa kutumia plau. # kuchimba "kulima kwa plau" # kwa ajili yako "nyuma yako" wakati wa kulima kwa plau, mtu huongoza ng'ombe akiwa nyuma yake.