# Maelezo ya jumla Yahweh anaendelea kumtia changamoto Ayubu # Je waweza kuwinda... kulala katika hali ya kuvizia Yahweh anatumia maswali haya kukazia kwamba yeye anajua jinsi ya kulisha simba, lakini Ayubu hajui. # mawindo "nyara" Huyu ni mnyama ambaye anaweza kuliwa na simba # simba jike Huenda ni "simba" # au kutosheleza hamu ya watoto wadogo wa simba "au kuwapa simba wadogo chakula cha kutosha ili kwamba waweze kuishi" # watoto wake wadogo "simba wadogo." Hawa ni simba wadogo ambao wana umri unaotosha kuwinda wao wenyewe. # katika pango lao "katika sehemu ambazo wanaishi" au "sehemu za makao yao" # kukaa katika kificho "kulala katika uoto wa mimea minene" # kulala katika hali ya kuvizia "ambayo ni sehemu ya kuvizia" au "ni sehemu ambayo wanajificha ili kukamata wanyama wengine." Simba hujificha katika katika mimea minene na kusubiria mnyama apite na ili wamrukie na kumkamata mnyama huyo.